jog

jog

Sunday, October 5, 2014

KICHEKELEO:HUYU NAE

MGONJWA:Dokta kuna ndoto inanijia kila usiku naomba msaada wako
DOKTA: Unaota nini?
MGONJWA: Dokta naona mademu masupasta wote wa bongo wanapigania kunibaka, me napigana nao nawatandika mangumi mpaka wanakimbia wote
DOKTA: Sasa watakaje ndugu yangu
MGONJWA: Dokta tafadhali nikate hii mikono

Wednesday, October 1, 2014

KICHEKELEO:MMMH HAYA MAISHA NI SOOO

JAMAA WAWILI MMOJA TAJIRI NA MWINGINE MASKINI WAKO DUKANI WANANUA ZAWADI KWA AJILI YA WAPENZI ZAO:

Maskini:vip mwenzangu wamnunulia nini mamsap?

Tajiri:mi namnunulia pete ya almasi  na gari kali la milioni mia moja

Maskini:hee kwanini unamnunulia vyote hivyo si ungemnunulia kimoja?

Tajiri:ILI ASIPOPENDA ALMASI aendeshe gari??vip wewe mwenzangu wamnunulia nini

Maskini:mimi namnunulia KANDAMBILI  pamoja na sumu ya panya,ili aispopenda kandambili nimwambie akafie mbele



MAPICHA:we mwanya na kicheko mweeeee

POMBE NI HATARII

JAMAA KALEWA KINOMA akawa anajikongoja kwenda nyumbani mdogo mdogo huku akitambaa 
ghafla akasimamishwa na askari doria

ASKARI:mZEE UMELEWA sana inabidi nkukodie tax ikupeleke nyumbani kwani sa hizi hutakiwi kuwa barabarani si salama

MZEE:kwani polisi unauhakika gani kuwa nimelewa ?

ASKARI:mzee mi ni mtaalam wa mambo haya na niamini mimi kuwa umelewa sana

MZEE:yaaaani we polisi unauhakika au unafurahisha tu jamii

ASKARI:Ninauhakika na pia usinipotezee muda twende>>>.......

MZEE:ooooooph !!!!!!!!!!!!Mungu mkubwa kumbe nimelewa,nilidhani mimi ni kiwete

WAUEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!

JAMAA kaingia bar akaagiza mzinga wa konyagi kisha akaanza kuufakamia haraka haraka kama anawahi sehem>>>>

WEITA:He wewe mbona unafakamia pombe kiasi hicho?

JAMAA:Yaani hata wewe ungefanya ninachofanya endapo ungekuwa na mawazo hivi?

WEITA:Hali gani jamani,mawazo ni sehemu ya maisha hebu niambie nikusaidie

JAMAA:Yaani hapa nina jero tu mfukoni nawaza huu mzinga ntaulipiaje

 

Monday, January 13, 2014

KICHEKO:ACHA NI CHEKE MIE

Siafu wanne walikuwa katika matembezi wakakutana na tembo;
SIAFU 1: Tumuuwe
SIAFU 2: Hapana tumvunje miguu tu
SIAFU 3: Tumsukume pembeni atupishe tupite
SIAFU 4:Hapana tumwache tutakuwa tunamuonea sisi tuko wanne ye yuko peke yake, ITAKUWA DHAMBI

CHEKAAAAAAAA KIDOGO



Yanki mmoja alikuwa na mke wa mtu, tena nyumbani kwa mwanamke yule wakati mwenye mali  yuko kazini. Mvua kubwa ikaanza hali ya hewa ikawa nzuri zaidi na wazinzi hawa wakawa wanafurahi zaidi, ghafla mke akasikia gari la mumewe, akamwambia mpenzi wake, 'Amka haraka tokea dirishani jamaa atatuua wote'. Jamaa si akaanza ubishi, eti ohh ntatokaje nje na kuna mvua?,  mke akawa mkali,' Pumbavu mkubwa, akiingia humu ni kifo wewe'. Basi jamaa akachukua nguo zake na kujitosa nje kupitia dirishani na kutokomoea vichochoroni. Ile anaingia barabara kubwa akakutana na kundi kubwa la watu wanakimbia mchakamchaka nae akajiunga humo. Jamaa wakawa wanamshangaa, mmoja akammuuliza,' Mbona unakimbia mchakamchaka uchi?' Muasherati akajibu, 'Unajua huwa napenda kukimbia hivi inasaidia kiafya'. Akaulizwa tena, 'Yaani ndio ukimbie umevaa kondom?'. Jamaa bila wasiwasi akajibu, 'Hii nimevaa kwa kuwa leo kuna mvua '