Kajamaa ambako hakajawahi kusafiri kwa boti kalilazimika kwenda na boti
Zanzibar. Kakaa kwenye kiti karibu na dirisha, kabla safari haijaanza,
bonge mmoja akaja kukaa pembeni ya kale kajamaa. Safari ikaanza,
haukuchukua mda mrefu Bonge akawa anakoroma. Kamjamaa si kakaanza
kusikia kichefuchefu, kakawa kanaogopa kumwamsha Bonge ili kapite
kakatapike chooni, na kumruka Bonge pia kakawa hakawezi. Kakajitahidi
kujikaza lakini bahati mbaya boti ikarushwa na wimbi kakashindwa
kujizuia kakaachia tena kakamtapikia Bonge kifuani. Bonge akstuka
akaamka akakuta matapishi kwenye shati na suruali yake, wakati Bonge
bado anashangaa, Kamjaa kakawahi;
KAMJAMAA: Pole, vipi unajisikiaje sasa?
KAMJAMAA: Pole, vipi unajisikiaje sasa?
No comments:
Post a Comment