Yanki mmoja alikuwa na mke wa mtu, tena nyumbani kwa mwanamke
yule wakati mwenye mali yuko kazini. Mvua kubwa ikaanza hali ya hewa
ikawa nzuri zaidi na wazinzi hawa wakawa wanafurahi zaidi, ghafla mke akasikia
gari la mumewe, akamwambia mpenzi wake, 'Amka haraka tokea dirishani jamaa
atatuua wote'. Jamaa si akaanza ubishi, eti ohh ntatokaje nje na kuna
mvua?, mke akawa mkali,' Pumbavu mkubwa, akiingia humu ni kifo wewe'.
Basi jamaa akachukua nguo zake na kujitosa nje kupitia dirishani na kutokomoea
vichochoroni. Ile anaingia barabara kubwa akakutana na kundi kubwa la watu
wanakimbia mchakamchaka nae akajiunga humo. Jamaa wakawa wanamshangaa, mmoja
akammuuliza,' Mbona unakimbia mchakamchaka uchi?' Muasherati akajibu, 'Unajua
huwa napenda kukimbia hivi inasaidia kiafya'. Akaulizwa tena, 'Yaani ndio
ukimbie umevaa kondom?'. Jamaa bila wasiwasi akajibu, 'Hii nimevaa kwa kuwa leo
kuna mvua '